Tetesi zinasema Manchester United ina matumaini ya kumsajili winga wa England Jadon Sancho, 20, kutoka Borussia Dortmund kwa kima cha chini ya pauni milioni 100 mwaka huu.
Tetesi zinasema Liverpool imebadilisha msimamo wake kwa ajili ya winga wa Uswisi Xherdan Shaqiri, 29, na haitamruhusu kuondoka mwezi huu.
Kocha mpya wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino amehusishwa na kutaka kuwasajili wachezaji wawili waliokuwa Tottenham – kiungo wa kati wa England Dele Alli, 24, na mchezaji wa Inter Milan raia wa Denmark Christian Eriksen, 28.

Arsenal imejiunga na vilabu vingine vya Ligi ya Premier ambavyo vimeonesha nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Celtic raia wa Scotland Ryan Christie, 25, ikiwa na matumaini kwamba aliyekuwa beki wa kushoto wa timu hiyo Kieran Tierney, 23, atafanikiwa kumshawishi kiungo huyo kuingia uwanja wa Emirates.
Tetesi zinasema Mikel Arteta hana uhakika ikiwa kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil atarejea kikosini. Mchezaji huyo, 32, hakuchezea Arsenal msimu huu.
Tetesi zinasema AC Milan na Paris St-Germain wanataka kumsajili winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 28, katika dirisha hili.
Tetesi zinasema Borussia Dortmund imeonesha nia ya kumchukua winga wa Manchester City, 18, Mholanzi Jayden Braaf.

Mlinzi wa Arsenal Rob Holding, 25, anakaribia kufikia makubaliano mapya ya muda mrefu, na kumaliza matumaini ya timu nyingine kubwa kubwa zilizokuwa zinapania kumchukua kwa mkopo.
Tetesi zinasema mchezaji wa USA DeAndre Yedlin, 27, huenda bado akasalia Newcastle msimu huu licha ya mazungumzo ya kuondoka mnamo mwezi huu.
Kocha wa Everton Carlo Ancelotti hata mzuia mchezaji yeyote ambaye anataka kuondoka klabu hiyo mwezi huu lakini anasema hakuna ambaye ameonesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Uturuki, 29, Cenk Tosun.
Juventus inafikiria kumnunua mshambuliaji wa klabu ya Shandong Luneng, Graziano Pelle, 35, aliyewahi kuichezea Italia ambaye pia amehusishwa na West Ham.
Tetesi zinasema Kocha Nuno Espirito Santo anasema Wolves iko tayari kufanya maamuzi kipindi cha usajili wa wachezaji Januari.
Brighton haitarajii kuuza mchezaji yeyote muhimu Januari, licha ya matatizo ya kifedha ambayo yametokana na ugonjwa wa virusi vya corona lakini baadhi ya wachezaji katika kikosi chake huenda wakaondoka kwa mkopo.

Dundee United imewasilisha ombi la kumtaka mchezaji wa klabu ya Airdrieonians, 20, mshambuliaji wa Ufaransa Thomas Robert, ambaye pia amehusishwa na kuhamia Rangers na Celtic.
Tetesi zinasema Wolves inaongoza West Brom na Fulham katika mbio za kutaka kumsajili mlinzi wa Grimsby, 19, Mattie Pollock.
Tetesi zinasema mlinzi wa Aston Villa Bjorn Engels, 26, amehusishwa na kurejea Ubelgiji mwezi huu.
Shirikisho la kandanda (FA) limeonya vilabu kuwa ni lazima vitimize michuano ya raundi ya tatu ya kombe la FA Cup wiki ijayo hata kama wachezaji wanaopatikana na waliothibitishwa kutokuwa na virusi vya corona ni 14 pekee.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?



Adelta
Tetesi zinasomeka
Rahmal
Tetesi ziko poa
warda
United wakituwekea huyu biashara imeisha ni ushind kila siku
Sarah
Zimeeleweka tetesi
Magdalena
United wajipange
Caroline
Asante kwa taarifa
Tatu
Habari nzuri
Issa
Sancho. Njoo man
Sania
Asante kwa tetesi bomba meridianbet
Saupha mohamed
Goodnews
Chiku
Tetesi za kukata na shoka
Dorophina
Itakuwa poa sana kama man u wakifanikiwa kumsajili sancho
Ernest Kimeru
Ngoja tuone
Mwanahamisi
Gud news
Hopemwaikuka
Carlo yuko sahihi
Neema juma
Tetesi ziko poaa
Lydia Emmanuel Magoti
Ngoja tuone
Angelina
Nice update
Sabrina
Taarifa timamu
felister
ngoja tuone