Lakers na Bucks Mambo ni Bambam!!

La Lakers wameondoka na ushindi kwa mara ya pili mfululizo wakati ambapo Milwaukee Bucks wamewagaragaza Chicago Bulls usiku wa kuamkia leo.

Lakers walikuwa uwanjani kuchuana na San Antonio Spurs ambapo vijana wa LA wameibuka na ushindi wa pointi 109-103.

LeBron James alimaliza mchezo kwa kuweka ‘tripple-double’ hii ni akiwa amefunga pointi 26, alitoa pasi 10 za magoli na kucheza mipira 11 iliyokufa.

Anthony Davis (kushoto) na LeBron James (kulia)

Anthony Davis ndio alikuwa shujaa wa Lakers safari hii akipachika pointi 34, na kucheza mipira 11 iliyokufa. Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa vijana wa Los Angeles mbele ya Spurs ndani ya siku tatu.

Kwingineko kunako matokeo ya NBA, Milwaukee Bucks wamewalaza chali Chicago Bulls kwa ushindi wa pointi 126-96.

Giannis Antetokounmpo (katikati) akipambana na wachezaji wa Chicago Bulls.

Giannis Antetokounmpo alipachika pointi 29, alitoa pasi 8 na kucheza mipira 12 iliyokufa. Hakuna timu iliyofunga pointi nyingi kwa mipira ya adhabu (108) kuwazidi Bucks mpaka sasa kwenye msimu huu.

Matokeo ya michezo ya NBA iliyochezwa Ijumaa usiku.

Memphis Grizzlies 108-93 Charlotte Hornets, Detroit Pistons 96-93 Boston Celtics, Dallas Mavericks 93-83 Miami Heat, Atlanta Hawks 114-96 Brooklyn Nets, Washington Wizards 130-109 Minnesota Timberwolves, Phoenix Suns 106-103 Denver Nuggets, Utah Jazz 106-100 Los Angeles Clippers, Portland Trail Blazers 123-98 Golden State Warriors


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?

SOMA ZAIDI

17 Komentara

    Nawakubali Sana Lakers

    Jibu

    NBA kuzuri

    Jibu

    Hongera zao

    Jibu

    Lakers wapo vizuri

    Jibu

    Lakerson fire

    Jibu

    Ongera kwao

    Jibu

    Wapo vizuli

    Jibu

    NBA kumekucha

    Jibu

    Mambo moto

    Jibu

    Lakers wapo vizuri sana

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Wapo vizuri

    Jibu

    Kwa raha zao

    Jibu

    Wapo vizuri

    Jibu

    Lakers chama langu

    Jibu

    Lakers wapo vizuri

    Jibu

    Kwa raha zao

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.