Tetesi zinasema mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo, 31, anafikiria kuhamia katika ligi ya Marekani ya MLS. Uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Man United kutoka kwa klabu ya China ya Shanghai unakamilika mwisho wa mwezi huu.
Tetesi zinasema Tottenham huenda isiongeze mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 31, kutoka Real Madrid kwa msimu wa 2021-22.
Beki wa Brighton Tariq Lamptey, 21, anakaribia kuandikisha mkataba wa kandarasi ya muda mrefu na klabu hiyo Ligi ya Uingereza. Bayern Munich ni miongoni mwa klabu ambazo zinahusishwa na uhamisho wa beki wa England wa timu ya wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 21.

Tetesi zinasema mshambuliaji wa Brazil Neymar, 28, ameanza mazungumzo ya kuongeza kandarasi yake katika klabu ya Paris-St Germain.
Tetesi zinasema Tottenham na Chelsea zina hamu ya kumsajili beki wa kati wa Korea Kusini mwenye umri wa miaka 24 Kim Min-jae, ambaye anachezea klabu ya china ya Beijing Guoan.
West Ham inafikiria kumsajili mshambuliaji na wanamlenga mshambuliaji wa klabu ya Reims na Senegal Boulaye Dia, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 akipatikana kwa dau la £15m.
Tetesi zinasema Aston Villa ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Bournemouth na Wales David Brooks, 23, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.
Klabu ya RB Leipzig haifikirii kumuuza beki wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 Dayot Upamecano licha ya kwamba anaweza kuondoka katika majira ya joto kwa dau la £37.4m. Liverpool, Chelsea, Manchester United na Bayern Munich ni miongoni mwa timu zinazomnyatia.

Tetesi zinasema beki wa kulia wa Aston Villa na Ufaransa Frederic Guilbert, 26, amekataa uhamisho wa kueleka katika klabu ya Uturuki ya Istanbul Basaksehir.
Arsenal ni miongoni mwa klabu zinazomuwania winga wa klabu ya Shakhtar Donetsk na Israel Manor Solomon, 21, wakiwa na lengo la kuwasilisha ombi kwa klabu hiyo ya Ukrainian katika majira ya joto.
Joan Laporta, Víctor Font na Toni Freixa ndio wagombea waliosalia katika kuwania wadhifa wa urais katika klabu ya Barcelona . Uchaguzi huo utafanyika siku ya Jumapili, tarehe 24.
Mshambuliaji wa Uholanzi Klaas-Jan Huntelaar, 37, huenda akarudi katika klabu ya Schalke. Mshambuliaji huyo aliondoka katika klabu hiyo ya Ujerumani na kuelekea Ajax mwaka 2017 ambapo alihudumu kwa muda wa miaka saba.
MERIDIANBET INAKUPA NAFASI YA KUWA MILIONEA KWA KILA BAADA YA DAKIKA 5
Mchezo wa Keno unakupatia fursa ya kuibuka kidedea kupitia droo zinazochezwa kila baada ya dakika 5 tu!! Tunaposema Meridianbet ni nyumba ya mabingwa, tunamaanisha!!



Ernest Kimeru
Dayot Upamecano ndio habari ya mjini kwasasa
Sania
Tetesi bomba meridianbet
Shakila mrope
Habari njema meridian bert mko makini
Hopemwaikuka
Ziko vzur sana
Magdalena
Spurs naona wanataka kutengeneza kikosi kipana
Caroline
Asante kwa taarifa
Flomena
Good news
Khadija
Habari njema sana kwa wapendwa wa meridian
Sarah
Kalii
Dorophina
Nice update
Rahmal
Tetesi ziko poa
Angelina
Nice update
warda
Zilikuwa poa