Tetesi zinasema kuna uwezekano mkubwa Cristiano Ronaldo, 36, akarejea tena Manchester United kuliko Madrid akiamua kuondoka Juventus msimu huu.
Nyota wa NBA LeBron James ameungana na Fenway Sports Group, ambayo inamiliki Liverpool – klabu ambayo amekuwa akiwekeza hisa zake tangu mwaka 2011.
Tetesi zinasema Liverpool wanatafakari uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Norway Sander Berge, 23, kutoka Sheffield United.
Tetesi zinasema Manchester United wamezungumza na ajenti wa mlinzi wa Fiorentina na Serbia Nikola Milenkovic, 23.

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ameupatia umuhimu mpango wa kumsaini mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, kutoka Borussia Dortmund msimu huu kuwa mkakati wake binafsi.
Winga wa Sporting Lisbon na Pedro Goncalves, 22, huenda akajiunga na Manchester United ikiwa klabu hiyo itashindwa kumleta Old Trafford kiungo wa kimataifa wa England Jadon Sancho ,20, kutoka Borussia Dortmund.
Tetesi zinasema mpango wa Manchester United kumsaka mlinzi wa Sevilla Jules Kounde, 22, umekuwa rahisi baada ya klabu hiyo ya Uhispania kupunguza bei ya Mfaransa huyo hadi £50m.

Kiungo wa kati wa Arsenal Matteo Guendouzi, 21, amesema atafanya kazi kwa bidii kurejea katika mpango wa Mikel Arteta baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika Hertha Berlin mwisho wa msimu huu.
Tetesi zinasema Tottenham wanapania kumuuza mchezaji wa kimataifa wa Colombia, Davinson Sanchez ,24, na tayari wameanza kutafuta mbadala.
Tetesi zinasema Chelsea wamehusishwa na uhamisho wa kiungo wa kati wa Palmeira, Gabriel Menino kutoka Brazil ambaye pia ananyatiwa na Atletico Madrid.
Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, 39, amekubali kurejea katika kikosi cha timu ya taifa ya sweden na anatarajiwa kusaini mkataba mpya AC Milan.
Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.



Lydia Emmanuel Magoti
Ziko poa
Sarah
Ziko bomba
Caroline
Safiiii
Dorophina
Itakuwa balaa Ronaldo kurejea man u
Venerose
Asanteni kwa makala
Adelta
Ziko poa
Mwanahamisi
Safi
Hopemwaikuka
Zmekaa poa
warda
Akija Man U nitafurahi sana