Klabu ya Simba SC imeliomba Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) wawaruhusu kuingiza mashabiki kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita ambao utapigwa April 03 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Huu ni mchezo muhimu ambao Simba SC inahitaji kushinda au hata matokeo ya sare kuweza kutinga robo fainali.

Mchezo dhidi ya Al Merrikh, Timu hiyo ilipewa ruhusa ya kuingiza mashabiki 200.
CAF imeiruhusu Al Merrikh kuingiza mashabiki 1000 katika mchezo wao dhidi ya Al Ahly hivyo yapo matumaini kwa Simba nao kupewa ruhusa hiyo ingawa yawezekana idadi isiwe kubwa.
Hata hivyo mnyama amejipanga kushinda mchezo huo bila ya kujali uwepo wa mashabiki kama ilivyokuwa mchezo uliopita dhidi ya Al Merrikh.
Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.



Adelta
Itakuwa Jambo zuri kurudisha mashabiki
Venerose
Kweli kabisa mashabiki tuna umuhimu sana
Caroline
Asante kwa taarifa
Sarah
Mpira bila mashabiki haunogi
neema juma
Mashabikii lazima wakubaliwe kwenda uwanjanii
Lydia Emmanuel Magoti
Itakuwa poa
warda
Itakuwa poa sana