Mchezaji kinda wa Azam, Pascal Gaudence Msindo ameweka rekodi katika ligi kuu ya tanzania bara VPL, yakuwa mchezaji mdogo kucheza katika ligi hiyo, Miaka 17 na miezi 8.
Pascal Msindo pia aliibuka mchezaji bora katika mashindano ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya Umri wa miaka 20 (Afcon U20) kwa Kanda ya CECAFA yaliyofanyika Arusha mwaka jana.

Azam FC walimuanzisha Pascal Msindo katika kikosi dhidi ya JKT Tanzania ugenini jana kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kucheza Ligi Kuu mwaka huu.
Msindo anayecheza nafasi ya beki wa kushoto, ana umri wa miaka 17 na miezi nane (8) akiwa amezaliwa Agosti 17, 2003 na leo amecheza kutokana na timu yake kumkosa Bruce Kangwa anayetumikia adhabu ya kukosa mechi tatu baada ya kupata kukusanya kadi tatu za njano.
Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.



Adelta
Vizuri Sana
Sarah
Safii
dorophina
Pongezi kwake
warda
Sasa alifanya vizuri?