Indonesia wanatamani mashindano ya Olympic yafanyike nchini mwao. Nchi hii ambayo kwa sasa inaendesha mashindano makubwa kabisa ya michezo Asia wanatarajia kuingia katika kuwania nafasi ya kufanya mashindano hayo. Raisi wa nchi hiyo, Joko Widodo ametangaza baada ya kukutana na raisi wa kamati ya kimataifa ya Olympic (IOC) bwana Thomas Bach.
Nchi zingine zinazovutiwa kukaribisha mashindano hayo ni India, Australia na China. Raisi Widodo anasema kwa kutumia uzoefu walioupata katika michezo ya Asia (Asia Games) wanaamini kwa sasa wanaweza kufanya tukio kubwa zaidi la michezo katika nchi hiyo.
Zaidi ya wanamichezo 12,000 kutoka nchi 45 wapo nchini Indonesia kushiriki michuano ya michezo ya aina zaidi ya 60 inayoendelea nchini humo. Thomas Bach ameikaribisha nchi hiyo akiamini uzoefu wa Asian Games, na mafanikio makubwa waliyoyapata katika michezo hiyo ni msingi mzuri kwa mashindano Olympic 2032.


Povel tz
Hongera kwao