Klabu ya Sunderland wamevunja mkataba wa Papy Djilobodji ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa ada ya paundi milioni 8. Klabu hiyo inadai sababu ya kuvunja mkataba huo ni Papy kurudi akiwa amechelewa na hayuko sawa kiafya.
Djilobodji raia wa Senagal mwenye umri wa miaka 29, alitokea Chelsea miaka miwili iliyopita. Alishindwa kurejea kwa wakati katika klabu hiyo baada ya kuchukua likizo ya bila malipo mwezi Julai.
Klabu ya Sunderland inadai staa huyu alishindwa kabisa vipimo vya afya ambavyo kila mchezaji alihitaji kufaulu ili andelee kupiga soka. Imekuwa vigumu kwa klabu hiyo kumpokea katika hali aliyonayo baada ya kushindwa vipimo vya afya ambavyo wenzake katika klabu hiyo walifanyiwa ukiacha kuchelewa na kupuuzia wito kurudi klabuni hapo mara kadhaa.
Mkataba wa Djilobodji ulikuwa unaisha mwaka 2020, alipaswa achukue likizo yake hadi mapema Agosti lakini alirejea klabuni hapo wiki ya kwanza ya mwezi Septemba.


Khadija
safi meridian#meridianbettz