Unapokuwa umepata kazi sehemu, siku zote inabidi uwaoneshe mabosi wako kwamba wewe ni mstaarabu na utakuwa mwema, lakini haikuwa hivyo kwa Memphis Depay ambaye amesainiwa na Barcelona juzi tu!
Depay alitakiwa kutangazwa rasmi na Barcelona kama usajili rasmi wa klabu hiyo, lakini mchezaji huyo alienda zake likizo moja kwa moja baada ya timu yake ya Uholanzi kuondolewa kwenye 16 bora na Czech Republic.
Depay amesajiliwa na Barcelona akitokea Lille ambapo alidumu kwa miaka 4 toka aondoke United mwaka 2017, ambapo hakuwa na msimu mzuri sana kutokana na kukosolewa kwa kila kitu alichofanya.
Hivi karibuni mchezaji huyo alinukuliwa kueleza kuwa huwa hapendi sana kusemwa kwenye maamuzi yake hususan kwenye masuala ya kwenda likizo au kutumia pesa sana kwani huwa anatumia pesa alizotengeneza mwenyewe kwa jasho lake!
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

