Hatimaye hamu ya mashabiki wa Manchester United kuona mwisho wa sakata la usajili wa Jadon Sancho, imetimilika. Sancho ni rasmi mchezaji wa United.
Kwa miaka minne mfululizo, Man United imekuwa ikipambana kuisaka sahihi ya Sancho bila mafanikio lakini mwaka huu – IMEWEZEKANA!
Jadon Sancho anatua United kwa usajili wa £73M akitokea Borussia Dortmund ambapo aliitumikia klabu hiyo kwa misimu minne. Akiwa Dortmund, Sancho alipachika jumla ya magoli 50 na kutoa pasi 64 za magoli.

Ole anasema” uwezo wake (Sancho) wa kufunga na kutoa pasi za magoli unajieleza wenyewe. Ataongeza kasi, burudani na ubunifu kwenye mfumo wetu wa uchezaji”
Sancho amenukuliwa akisema ” Nafasi ya kujiunga na Manchester United, ni ndoto iliyotimia, ninasubiri kwa hamu kuonesha uwezo wangu kwenye EPL“.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!



Ernest
Bado sakata la Pogba sasa