Klabu ya Real Madrid inaripotiwa kuwa kwa sasa imeachana na hofu ya kumpoteza nyota wake Raphael Varane baada ya staa huyu kutajwa kukubaliana masharti binafsi na klabu ya EPL.
Nyota huyu wa Ufaransa ambaye amekuwepo Bernabeu kwa takribani misimu 10, sasa anatarajia kumaliza mkataba wake kwa kipindi cha takribani chini ya mwaka mmoja.
Verane anadaiwa kuwa anashinikiza kuondoka ili akapate changamoto mpya mahalki pengine, Manchester United wakihusishwa na kufanya makubaliano ya masharti binafsi na staa huyu.
Hata hivyo, Real Madrid, ambao wanapenda kusalia na Varane bado wanatarajiwa watataja dau kubwa bila kujali hali yake ya mkataba ya sasa.
Kwa mujibu wa Daily Mail, Real Madrid wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha staa huyu anasaini mkataba mpya, lakini kwa sasa wameamua kumuacha atimize mapenzi yake ya kwenda Old Trafford.
Taarifa zinasema tayari ameshafanya makubaliano ya awali ya mkataba wa miaka 5 baada ya kumalizana na Real.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!
Ernest
Ngoja tuone kama watu watavunja vibubu