Saa chache zilizopita mchezaji wa kike Lauren James amefanikisha uhamisho wake kutoka timu ya wanawake ya Manchester United kwenda timu ya wanawake ya Chelsea ambapo ndipo alipoanza maisha yake ya soka.
Lauren anajiunga na Chelsea kwa dili la miaka minne ambapo pia ndipo anapocheza kaka yake Reece James katika nafasi ya beki.

Katika ukurasa wa mchezaji huyo ambaye alifanikiwa kung’aa sana akiwa na United msimu uliopita, ameonesha furaha yake, huku akieleza kuwa anafuraha sana kurudi nyumbani ambapo alianza kazi yake rasmi.
Akiwa na United, Lauren James amefanikiwa kufunga magoli 14 katika mechi 18 alizocheza na kuisaidia United kuingia katika ligi kuu, kitu ambacho kilipelekea kuitwa timu ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 19.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!



Ernest
Imekaa pouwa sana hii