Mchezaji wa Chelsea, Marcos Alonso anaripotiwa kuishinikiza Chelsea imruhusu kuondoka klabuni hapo ili akapate changamoto mpya huko Serie A akiwa na Inter Milan.
Mchezaji huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 30 sio mgeni sana katika mpira wa miguu wa Italia, akiwa amecheza Fiorentina kutoka 2013 hadi 2016.
Marcos amekuwa akiteseka kupata muda wa kucheza na Chelsea hususan uwepo wa mtu kama Emerson Palmieri, ambaye amekuwa akihusishwa na Napoli.
Alonso alikuwa tayari aliwahi kuhusishwa na Inter kama sehemu ya dili la Chelsea kwa Achraf Hakimi, lakini hiyo haikutimia, kwani beki huyo wa pembeni alikwenda Paris Saint-Germain badala yake.
Kulingana na La Gazzetta dello Sport, Chelsea wanaomba € 15-20m kwa Alonso, wakati Inter ingependelea mkopo na chaguo la kununua.
Inaripotiwa nchini Italia kwamba Marcos analazimisha Chelsea kumruhusu aondoke, lakini mkataba wake unaendelea hadi Juni 2023.
Klabu hiii ya Uingereza ililipa € 23m kusaini Alonso kutoka Fiorentina mnamo 2016.
Roma pia ilikuwa imeonyesha nia, kabla ya kukubaliana na Palmeiras kwa Matias Viña badala yake.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!



Ernest
Alonso amekuwa hana namba ya kudumu ndani ya Chelsea ndio mana hana furaha