Manchester City wanahusishwa na saini ya nyota wa wa Tottenham, Harry Kane. Kwa mujibu wa ripoti Man City wapo tayari kucheza mchezo wa ngoja ngoja katika kuiwinda saini yake.
Nyota huyu wa mda mrefu Spurs, tayari alishauambia uongozi wake kuwa anataka kupata changamoto mpya mahali pengine, baada ya kushindwa kutwaa mataji muhimu na Spurs.
Wakati Man City wakionesha kuwa na nia thabiti ya kumsajili staa huyu, Tottenham wanatajwa kuwa hawapo tayari kupokea kiasi chochote chini ya £160m.

The Sun inaripoti kuwa City wapo tayari kuendelea kusubiri juu ya suala hilo hadi kufungwa kwa dirisga ka uhamisho ili wafahamu upepo unaelekea wapi, na wao wafanye maamuzi.
Wakati huo, Spurs wanaamini ikiwa ikiwa SPurs hawatataka kuwasilisha ofa rasmi mapema basi hiyo itavivutia vilabu vingine kuwasilisha ofa na wao watazingatia ofa inayokidhi vigezo vyao vya awali.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!



Ernest
Itafahamika tuu