Klabu ya Yanga SC imepangwa kukutana na Rivers United kutoka Nigeria katika raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champion League). Mshindi wa jumla wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya Al Hilal ya Sudan au Fasil Kenema SC ya Ethiopia.
Klabu ya Azam FC kwenye kombe la shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup) hatua ya awali imepangwa kukutana na Klabu ya Horseed SC ya Somalia na mshindi wa jumla wa mchezo huo atakutana na klabu ya Pyramids FC kutoka Misri.
Klabu ya Biashara United katika hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) imepangwa kukutana na FC Dakhil ya Djibouti. Mshindi wa jumla wa mechi hiyo amepangwa kukutana na mshindi wa mechi kati ya Hay Al Wadi FC ya Sudan au Ahli Tripoli ya Libya.
Klabu ya Simba SC wataanzia raundi ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champion League) imepangwa kukutana na mshindi wa mchezo kati ya Jwaneng Galaxy ya Botswana au DFC 8ème Arrondissement ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Unaanzaje siku yako bila kuwa na pesa, Meridianbet kupitia kasino zake za mtandaoni inakupa sababu ya kufanya siku yako kuwa njema. Mchezo maarufu wa Tiki Reward unaweza kukufanya milionea. Cheza sasa kibingwa!



Sania+mapua
Ratiba ni nzuri kwa time zote
Sarah
Ratiba ni nzuri sana