Kiungo wa Tottenham Hotspurs, Tanguy Ndombele anaripotiwa kuwa amefanya mazungumzo na kocha mkuu Nuno Espirito Santo na mkurugenzi Fabio Paratici na kuweka wazi kuwa ana lengo la kufanya vizuri zaidi.
Staa huyu wa Ufaransa, alikuwa anahusishwa na nia ya kuondoka Tottenham Hotspurs katika dirisha la uhamisho la msimu wa joto, na mpaka sasa bado hajacheza mechi yeyote msimu huu.
Taarifa zinasema kuwa kwenye kikao chake na Nuno na Paratici, staa huyu aliweka wazi nia ya kupambania nafasi yake kwenye timu ya kwanza pale Spurs.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari Uingereza,Tanguy Ndombele anajiandaa kushiriki mechi dhidi ya Rennes kwenye Europa Conference League.
Kiungo huyu wa miaka 24 alifanya mazoezi na kikosi wiki hii, kimsingi yupo fiti kucheza mechi dhidi ya Crystal Palace wikiendi, lakini inaonekana hilo bado halijawa mpango wa Spurs kwa sasa.
Tanguy Ndombele amechangia magoli nane na asisti nane katika mechi 75 alizocheza toka alipohamia Spurs toka Lyon mwaka 2019.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


