Tangu ajiunge na Paris Saint-Germain, Sergio Ramos bado hajacheza mchezo wowote kwa timu hiyo hatohusika pia katika mchezo wa Jumamosi wa Ligue 1 dhidi ya Clermont Foot katika dimba Parc des Princes.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 35 ni kama hatocheza mechi za makundi katika Ligi ya Mabingwa ugenini huko Club Brugge Jumatano ijayo.
Kwa mujibu wa L’Equipe, Ramos atalazimika kusubirikwa muda kidogo kabla ya kufanya mchezo wake wa kwanza akiwa na PSG na gazeti la Ufaransa lianaripoti kwamba hajatajwa katika michezo miwili.
Ramos alijiunga na PSG akitokea Real Madrid kwa uhamisho wa bure wakati wa dirisha la usajili na alikuwa acheze mechi yake ya kwanza baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa klabu ilieleza katikati ya mwezi Agosti.
“Sergio Ramos amerejea mazoezini na anatarajia kucheza baada ya mapaumziko ya mechi za kiamataifa,” Taarifa ya PSG ilisomeka.
Lakini sasa Ramos ataendelea kupona taratibu kwaajili ya kuwa sawa kwa 100% PSG inajaribu kuepuka shida zozote zinazoweza kumpata.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


