Luka Modric: City Wapanga Foleni Kuiwinda Saini Yake

Mabingwa wa Uingereza Manchester Citywanaripotiwa kuwa wapo kwenye matazamio ya kufanya maamuzi ya kumfukuzia nyota waReal Madrid, Luka Modric.

Nyota huyu mwenye uraia wa Croatia, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 36, yupo katika miezi yake 12 ya mwisho ya mkataba wake Real Madrid. Kwa sasa staa huyu anafikiria juu ya hatma yake ya baadaye.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja nchini Hispania, Pep Guardiola anahitaji kumsajili staa ambaye anaweza kufikia viwango vya staa wa Barcelona Sergio Busquets, na Modric anaonekana kuwa mchezaji ambaye anaweza kuleta uwiano kwenye kikosi cha Guardiola.

Luka Modric: City Wapanga Foleni Kuiwinda Saini Yake
Luka Modric

Hata hivyo, City bado wana machaguo kibao ya washambuliaji klabuni hapo. Lakini taarifa zinataja kuwa Luka Modric ndiye atakuwa mchezaji mzuri kumrithi Fernandinho, ambaye mkataba wake unafika tamati msimu ujao wa joto.

Kuna taarifa kuwa Modric anatamani kumalizia soka lake huko Marekani, lakini man City wanatamani kumpatia mkataba ambao atautumikia kabla ya kwenda kuungana na timu ya New York City FC.

Luka Modric amecheza jumla ya mechi 392 toka alipojiunga na Real Madrid akitokea Tottenham Hotspurs mwaka 2012.


USHINDI KIGANJANI KWAKO!

Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.

Meridianbet Online Casino

INGIA MCHEZONI HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.