Lionel Messi kukosa mchezo wa Paris Saint Germain dhidi ya Metz Septemba 22 kwenye dimba la Saint Symphorien.
Messi aliyetolewa katika dakika 75 kwenye mchezo wa jumapili dhidi ya Lyon ambapo Paris walishinda 2-1 huku psg ikiendeleza mwanzo mzuri, PSG imeshinda mechi sita kwenye ligi huku ikiongoza kwa pointi 5 dhidi ya Marseille timu inayomfuata.

Lionel ambaye aliacha sintofahamu na mkufunzi wake baada ya kutolewa kwenye dakika ya 75, alifanyiwa vipimo na kukutwa na matatizo ya mfupa wa mguu wake wa kushoto.
Mkufunzi wa PSG Mauricio Pochettino alisema, “alichukua maamuzi ya kumtoa Messi pale tu, alipohisi kuwa kaumia baada ya kuona akijishika zaidi ya mara moja kifundo chake.”
Lionel mpaka sasa bado hajafunga goli kwenye ligi ya Ufaransa ‘Ligue 1’.
Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.


