Menejea wa mda wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ana imani juu ya mastaa wa klabu hiyo golikipa David de Gea na mshambuliaji Anthony Martial kuwa watasaini mkataba mkataba mpya na klabu hiyo.
Nyota hawa wawili walikuwa wakisuasua kusaini mikataba yao mipya huku klabu hiyo ikiamua kutumia makubaliano ya mikataba ya awali ya kuongeza mwaka mmoja kwenye mikataba yao.
Kwa kipindi cha hivi karibuni nyota hawa wameripotiwa kuwa wapo kwenye mazungumzo juu ya uwezekano wa kusaini mikataba yao mipya. Kwa mujibu Ole Gunnar kunaweza kuwa na taarifa niema kwa wapenzi wa Man Utd juu ya Martial na De Gea wiki chache baadae.
Ole Gunnar anatarajia kuutafuta ushindi wake wa nane toka alivyochukua kibarua cha Mourinho akiwa anaenda kuumana na Arsenal kwenye kombe la FA Ijumaa hii, anatarajia kazi ngumu na bora itafanywa na vijana wake wakiwemo De Gea ambaye amekuwa mkombozi baada ya kuokoa maduki mazito gemu zilizopita na Martial aliwa anakamilisha safu ya mbele. Ole Gunar anaamini vijana hawa lazima watabaki kwa kusaini mikataba mipya ya mda mrefu.
Wakati huo klabuni hapo, Scott McTominay tayari ameshaini mkataba mpya wiki hii, lakini wachezaji wengine kama Juan Mata, Ander Herrera na Ahley Young mikataba yao ikiwa inafika tamati mwisho wa msimu huu na haijafahamika kama wanasaini mikataba mipya au la!


isha
Duuh