Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC, Hitimana Thierry, amesema timu hiyo ilicheza kwa presha katika mchezo wa jana dhidi ya Polisi Tanzania lakini kupata alama tatu muhimu lilikua jambo la muhimu.

Hitimana amesema kitendo cha kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mabadiliko makubwa ya benchi la ufundi yalisababisha wachezaji kucheza kwa presha.
Kocha huyo ameongeza kuwa katika mchezo huo wapinzani wa kwanza walikuwa ni Simba wenyewe na Polisi walikuwa wa pili lakini kikubwa ni kupata ushindi.
“Tumetoka kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na tumebadili benchi la ufundi kwa hiyo tulikuwa na presha kubwa ndiyo maana nasema wapinzani wetu wa kwanza walikuwa sisi wenyewe,” amesema Hitimana.
Kuhusu mabadiliko ya wachezaji wanne katika kikosi yametokana na baadhi ya nyota wa Simba katika eneo la kiungo kuwa majeruhi.
“Taddeo Lwanga ni majeruhi na Jonas Mkude hakuwa fiti asilimia 100 ndiyo maana tumefanya mabadiliko yale kikosini ingawa nilitamani kuanza na washambuliaji wawili lakini kikubwa tunafurahi kwa ushindi,” aliongeza.
Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.

CHEZA HAPA

