Dirisha la Januari ndiyo limefika ukingoni, zipo klabu zilizoamua kuvunja vibubu na kuwaleta wachezaji wapya, wakati zingine zikiamua kubaki na nguvu ile ile. Pia, zipo zilizoamua kuwachukua wachezaji wapya kwa mkopo. Hapa kuna dondoo kwa ufupi sana katika kufunga dirisha la usajili la mwezi Januari.
Arsenal
Washika Mtutu bado wanaripotiwa kuwa wanajaribu kumsajili Christopher Nkuku kutoka PSG yakiwa yamebakia masaa kadhaa tu kufunga kwa dirisha la usajili, lakini dili hili lianaonekana kuwa gumu kufanikiwa.
Chelsea
The Blues wanaripotiwa kuwa bado walikuwa wanamuhitaji nyota wa Watford Abdoulaye Doucoure. Lakini Watford hawahitaji kabisa kumuuza mchezaji huyu ambaye anahusishwa na Chelsea.
Manchester United
Manchester United wanaripotiwa kuwa tayari wamekubali kumuuza Marouane Fellaini kuelekea kule klabu ya Uchina ya Shadong Lunebng. Nyotaa huyu anaripoeuwa kuwa pia amekubaliana na masharti ya mkataba wake mapema wiki hii.
Aston Villa
Villa wapo mbioni kukamilisha dili la mlinzi wa Bournemouth Tyrone Mings, nyota huyu kwa sasa yupo atafanyiwa vipimo na Aston Villa.
Southampton
Meneja wa Southampton amegusia kuwa Charlie Austin anaweza kusepa kama anaweza kupatikana mbadala wake.
Newcastle
Hawa wanatarajiwa kuthibitisha usajili wao wa kuvunja rekodi ya klabu wa Miguel Almiron kwa ada ya paundi milioni 20
Wolverhampton
Watabe hawa wanaripotiwa kuwa tayari wameshainasa saini ya Otto kwenye mkataba wa kudumu na klabu hiyo.


Povel
Habar njema