Wiki hii Ligi Kuu ya Uingereza imeshuhudia baadhi ya watabe wa EPL wakiwa na wiki ngumu, Liverpool wameshindwa kupata ushindi wakiwa wenyeji wa Leicester City kwenye gemu ya jana, Klopp anena sababu ya kuwashindwa Leicester City.
Wakati Manchester United wakiponea chupu chupu kwa kulazimisha sare ya bao 2-2 dhidi ya Burnley usiku wa Januari 29, Manchester City alikubali kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Newcastle United. Januari 30 imekuwa mbaya zaidi kwa Chelsea aliyechapwa bao 4-0, huku Liverpool akimaliza kwa kuruhusu sare ya bao 1-1.
Akielezea kwa nini Liverpool wameshindwa kuwachapa Leicester City wakiwa kwao, meneja Jurgen Klopp anasema kuwa Barafu iliyoanguka uwanjani humo ilikuwa ni moja ya sababu iliyopelekea ugumu wa gemu dimbani na kujikuta wakimaliza kwa sare kwenye gemu hiyo.
Klopp pia amegusia makosa ambayo anaamini yangekuwa yamebadilisha matokeo kama vile kunyimwa penati wakati kulikuwa na rafu aliyochezewa Keita na Pereira.
Leicester wamebahatika kuwa timu ya pili kuondoka bila kichapo pale Anfield msimu huu baada ya Man City kufanya hivyo oktoba 7 mwaka uliopita. Hata hivyo Liverpool wanaendelea kuwa vinara wakitofautana kwa pointi 5 na timu inayowafuatia Manchester City.


Furahav
Leicester wanajua
isha
klopp yuko vizuri