Hadi sasa kuna klabu ambazo zimetumia dirisha la usajili kuimarisha vikosi vyao, kwa kurudisha wachezaji wao waliokuwa kwa mkopo katika klabu nyingine na klabu nyingine zikiuza wachezaji wao ambao kwa upande mmoja au mwingine wameona wametosheka na huduma zao walizozitoa tayari. Baadhi ya klabu hizo ni;
Arsenal, wao wameweza kupata ingizo jipya ndani ya kikosi chao, japo mchezaji huyo ametua kwa mkopo kikosini hapo; lakini wamefanikiwa kumshawishi Denis Suarez kutoka Barcelona ambaye amekwishatua kwa washika bunduki hao. Suarez amehudumu chini ya Emery katika mechi 46 kipindi alipokuwa kwa mkopo Sevilla: katika msimu wa 2014/15 ambapo alufunga magoli 6 na kuisaidia Sevilla kunyanyua kombe la Europa. Na wamemtoa Emiliano Martinez kwenda Reading kwa mkopo.
Chelsea, wao wamefanya ingizo kubwa sana ambalo liliwafanya waingie kapuni kufanya usajili wake uliogharimu £57.6M. Christian Pulisic awali alikuwa anakipiga na Dortmund ambako ameamua kuachana nao na kujiunga na upande huo wa pili. Mchezaji huyo aliweza kusajiliwa na kubaki katika klabu hiyohiyo hadi msimu utakapokwisha. Hadi sasa ana magoli tisa katika mechi 28 alizocheza na timu yake ya taifa. Pia, wameongeza mshambuliaji katika kikosi chao ili kujifua zaidi na kuirudisha timu hiyo katika kipindi kile cha magoli mengi. Katika msimu wa 2015/16 akiwa chini ya Sarri alifanikiwa kufunga magoli 36. Pia amewaondoa Abdul Rahman Baba, Matt Miazga na Lewis Baker, Cesc Fabregas, Alvaro Morata na Victor Moses.
Liverpool, wao wamewarudisha kutoka kuhudumu kwa mkopo wachezaji wao Connor Randall na Ben Woodburn baada ya kuhudumu kwa mkpo katika klabu zao na kipindi hicho kuisha. Ikiwa ni sehemu ya kanuni za soka kuwa na idadi fulani ndani ya kikosi na kama ikitokea inazidi basi kutoa wachezaji hao kwa mkopo; pia wameweza kumtoa kwa mkopo Nathanial Clyne ambaye amekwenda Bournemouth na wakamuuza Solanke.
Manchestee City wao wameweza kufanya maingizo mapya ndani ya kikosi chao ikiwemo kumwongeza Ko Itakura kutoka Kawasaki Frontale (£990k) na Ante Palaversa; pia wameweza kuwarudisha kutoka kutumikia kucheza kwa mkopo vijana wao Anthony Caceres, Marlos Moreno. Hiyo ni dalili ya awali kabisa kwa klabu hizo kuweza kujiimarisha kwenye kinyang’anyiro cha ligi hiyo kwa sasa.
Manchester United hawajaona haja ya kusajili katika dirisha hili dogo wanajaribu kuweka hesabu zao vizuri kuona namna wanavyoweza kusajili kikosi kipana zaidi katika majira yanayofuata ambayo huwa na muda mrefu zaidi wa kuwatumia maskauti wao kupata wachezaji; vivyo hivyo kwa sasa mwalimu wa msimu wa kikosi hicho anajaribu kutumia wachezaji waliopo kwa kujaribu mifumo mbalimbali. Mbali na hilo amemrejesha nyumbani Joel Pereira kutoka Vitoria Setubal alikokuwa anaitumikia klabu hiyo kwa mkopo.
Povel
Gud news