Tunapozungumzia mafanikio katika soka, ni pale inapotokea mchezaji anaonesha mabadiliko kutoka katika hali aliyokuwa nayo hapo awali na kuanza kufanya vitu vikubwa katika jamii yake inayomzunguka. Mchezo wa soka umewatoa watu wengi sana kutoka kwenye hali duni walizokuwepo hadi kwenye ubilionea. Afrika haijaachwa mbali katika harakati hizo za kuwa na wachezaji wanaomiliki vitega uchumi vinavyowaingizia mapato makubwa. Wafuatao ni baadhi ya wachezaji wa kiafrika wanaomiliki mkwanja mrefu;
Samuel Eto’
Akiwa anashikilia rekodi ya kunyakua tuzo za mchezaji bora wa Afrika mara nne katika maisha yake ya soka, mchezaji huyo wa zammani wa Barcelona na timu ya taifa ya Cameroon anashikilia namba moja kwa kuwa na pesa ndefu kuwazidi wengine wa kiafrika kutokana na mafanikio aliyoyajenga akiwa kama mchezaji kwa kipindi chake. Akiwa na Anzhi Makhachkala aliweza kuvunja rekodi ya kulipwa mshahara mkubwa zaidi ambao ni $25M kwa mwaka kiwango ambacho ni kikubwa, kwa sasa anakipiga katika klabu ya Qatar. Utajiri wake unakadiriwa kufikia $95M kwa sasa huju akiwa na ndege binafsi, majumba ya kifahari, magari ya kifahari na kuchangia huduma mbalimbali za kijamii.
Didier Drogba
Ni aina ya washambuliaji hatari waliowahi kucheza ligi ya Uingereza na kuwa tishio duniani. Uwezo wake huo ulimfanya aweze kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa ndani ya klabu ya Chelsea miaka ya 2004 alipotua klabuni hapo akitoka Marseille. Mchezaji huyo alikuwa anavuna kitita cha $150,000 kwa wiki akiwa Chelsea, na alikaa klabuni hapo misimu nane. Mwaka 2012 aliweza kutimkia China ambako alikuwa analipwa $200,000 ambako alitengeneza kiasi kikubwa cha utajiri wake pia. Anakadiriwa kuwa na utajiri wa $80M.
Yaya Toure
Anakadiriwa kuwa na utajiri wa $70M na ni miongoni mwa viungo bora kutoka Afrika waliowahi kucheza soka la kulipwa nje ya nchi zao. Akiwa katika maisha ya soka alikuwa akipokea kitita cha €210,000 kwa wiki. Mbali na hilo mchezaji huyo amewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara nne kitu ambacho ni hatua kubwa kwa mwanasoka yeyote duniani. Kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake kuendelea kuitumikia Olympiakos ambayobalikuwa anahudumu kwa kipindi chote. Amecheza soka lake katika klabu kuwa nyingi kama Barcelona na Manchester City.
Hao ni baadhi tu ya wachezaji wanaoshikilia rekodi kwa Afrika kutokana na mafanikio waliyoyapata kutokana na soka. Wengine mbali na hao ni Emmanuel Adebayo, Michael Essien, Asamoah Gyan na Mikel Obi; ambao wamekuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa katika soka.


Issa
Habari nzuri