Cahill Amewakataa Juve, Monaco na Fulham!

Mlinzi wa Chelsea, Gary Cahill anakabiliwa na mda mchache wa gemu klabuni Chelsea chini ya meneja Maurizio Sarri. Taarifa za mapema mwezo Januari ziliripoti kuwa nyota huyu angekuwa anasepa klabuni hapo, klabu ya Juventus ndiyo klabu aliyohusishwa nayo sana huku klabu zingine za Monaco na Fulham pia zikiripotiwa kuwa zilikuwa zinamuwinda nyota huyu. Cahill anadaiwa kuwa amewakataa wote Juventus, Fulham na Monaco huku dilisha likifungwa akiwa amesalia Chelsea.

Sarri, ambaye pia kwa sasa hali ya uhusiano wake na kikosi chake inatia mashaka, alimruhusu mlinzi huyu kusepa katika dirisha la Januari. Hadi dirisha linafungwa nyota huyu hakuripotiwa kuwa amesainiwa na klabu yeyote kati ya zile zilizokuwa zikimuwinda katika dirisha hili dogo.

Kwa mujibu wa Skysports, Fulham wanaripotiwa kuwa tayari walishafanya mazungumzo ya dili la kudumnu na klabu ya Chelsea lakini nyota huyu yeye akakataa kukubaliana na masharti ya kujiunga na klabu hii.

Nyota huyu mwenye miaka 33 ambaye pia amekataa kuungana na mabingwa wa Serie A -Juventus na wale wa Ligue 1 -Monaco ili ajaribu kupambania nafasi yake klabuni hapo. Mkataba wa Cahill utakuwa unafika tamati mwisho wa msimu huu.

Akiwa klabuni Chelsea nyota huyu ambaye pia amewahi kukipiga pale Bolton na Aston Villa ameshinda mataji mawili ya EPL, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi ya Europa kwa kipindi cha miaka 7 alipokuwa klabuni hapo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.