Soka sio mpira tu kwa namna unavyochezwa uwanjani bali pia ni namna klabu hizo zinavyojilinda kwa kutengeneza mapato yanayochangia kuziendesha klabu zao. Kwa kiwango kikubwa klabu zinazotajwa mara nyingi ndizo zinazoshikilia rekodi hizo za kimapato. Utajiri huo mara nyingi hutokana na uzito wa vikosi vyao, mauzo ya vifaa vyao vya michezo, kufuatiliwa kwa kiwango kikubwa na hata vyanzo vya ndani vya mapato vya klabu husika.
Kwq mwaka 2019 mambo yamekuwa tofauti hasa kwa Madrid ambao toka 2017 wamekuwa wakishika nafasi ya kwanza katika kinyanganyiro hicho. Lakini kwa mwaka huu mambo yamebadilika kabisa kwao.
Manchester United
Kwa mwaka huu ameanza kwa kushika nafasi nzuri kwenye upande wa pesa pamoja na kuwa hayuko katika nafasi ya juu kwenye ligi hiyo. Utajiri wake unakadiriwa kuwa $827.9M, ambao unatokana na mikataba ya udhamini kama adidas, Chevrolet na nafasi yake ya kuchukua Europa mwaka jana imeleta athari chanya kwenye mapato kwaka huu,, haki za matangazo na kuguatiliwa kwa kiasi kikubwa duniani.
Real Madrid
Baada ya kukaa juu kwa kipindi kirefu kwa sasa wameachia nafasi hiyo kutokana na kuporokoka kwao katika utendaji hasa kuwa na matokeo mabovu yanayowafanya kukosa kwa kiasi kikubwa mapato ya ndani hasa uuzaji wa jezi na idadi ndogo ya mashabiki kufuatilia mechi zao viwanjani. Suala hili limewafanya washindwe kiendelea kuishikilia nafasi hiyo ya juu. Utajiri wao kwa sasa unakadiriwa kuwa $825.9M.
Barcelona
Kutoka kushikilia nafasi ya pili kwa kipindi kirefu kwa sasa ameweza kushuka sana hadi nafasi hii. Utajiri wake unatokana na masuala ya uwekezaji na udhamini kutoka kwa Nike na Qatar Airways ambao wanadhamini suala zima la vifaa vinavyotumiwa na miamba hao wa soka duniani. Taarifa za kiuchumi zinasema, kuondoka kwa Neymar klabuni hapo hakujaleta athari zozote kiuchumi ndani ya kikosi hicho na haziwezi kuathiri kitu kwa sasa. Wana utajiri wa $793.2M hadi sasa.
Pamoja na hao kuna vilabu vingine vinavyofanya vizuri upande wa mapato wakiwemo Bayern Munich nafasi ya nne wakiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia $719.8M, Manchester City nafasi ya tano akiwa na $646.2M, Arsenal nafsi ya sita akiwa na $597.1M, Paris Saint-Germain nafasi ya saba akiwa na $597.1M, Chelsea nafasi ya nane akiwa na $524.3M, Liverpool nafasi ya tisa akiwa na $519.5 na wanaofunga nafasi ya kumi ni Juventus walipanda haraka kimapato wakiwa na utajiri wa $496.9M hadi sasa.


Mariam mtandama
Safi
aisha
taarifa nzuri
Furahav
Inamana hata timu zetu za Afrika hakuna.
Issa
Safi sana
Povel tz
Noma sana