Klabu ya Chelsea ipo tayari kupeleka dau katika klabu ya Fenerbahce kwaajili ya kumsaliji beki wa kati wa klabu hiyo, Attila Szalai kulingana na ripoti mbalimbali.

Szalai, 23 amevivutia vilabu vingi barani ulaya baada ya kufanya vizuri katika mashindano yaliyopita ya Euro 2020 akiwa na timu yake ya Taifa ya Hungary.
Kulingana na taarifa mbalimbali katika vyombo vya habari vya michezo nchini Uturuki vinasema Chelsea wanaongoza katika mbio za kumsajili mchezaji huyo mwezi January baada ya kumfwatilia kwa muda.
Liverpool, West Ham, na Leicester City pia zimekuwa zikifwatilia kwa karibu mwenendo wa beki huyo anayefananishwa na Virgil van Dijk.
Taarifa pia zinasema Chelsea wapo tayari kutoa kitita cha £17m kwaajili ya beki huyo wa kati, Fenerbahce wanataka kumuuza mchezaji huyo ili kuweza kusajili wachezaji wengine katika kikosi hicho.
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?


