Baada ya kuamua kusitisha mkataba wa Dean Smith, Aston Villa wanapanga kufanya mazungumzo na makocha wawili.
Orodha ya wanaohusishwa na Aston Villa ni ndefu lakini, imeripotiwa kuwa miongoni mwao ni Roberto Martinez na Steven Gerrard.

Martinez anakiongoza kikosi cha Timu ya Taifa ya Ubelgiji ambapo kwa sasa, timu hiyo inajiandaa na muendelezo wa michezo ya kufuzu Kombe la Dunia 2022, Qatar.
Kwa Steven Gerrard, amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kuwa mrithi wa Jurgen Klopp endapo kocha huyo ataamua kuondoka Anfield siku yeyote. Hii ni kutokana na mahaba kati ya Liverpool na Gerrard ambaye aliitumikia klabu hiyo maisha yake yote ya uanamichezo.

Sasa hivi, Gerrard anaiongoza Rangers FC inayocheza Ligi Kuu nchini Scotland wakiwa kama mabingwa watetezi msimu huu. Akiwa na Rangers, wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi mbele ya Celtic FC ambao wameitawala ligi hiyo kwa takribani miaka 9 mfululizo.
Villa watafanikiwa katika mchakato wa kumpata kocha mwingine ndani ya wiki 2 kabla ya EPL kuendelea Novemba 20,2021?
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?


