Kinachoendelea miongoni mwa wachambuzi wa soka na mashabiki wa Man United kuhusu hatma ya Ole Gunnar Solskjaer, kwenye uongozi wa klabu hakupo hivo.
Shinikizo la Solskjaer kuondolewa klabuni hapo linaendelea kushika kasi nje ya United. Matokeo mabaya, timu kukosa muelekeo, kupendelea baadhi ya wachezaji, kuwanyima nafasi baadhi ya wachezaji, wachezaji wenyewe kwa wenyewe kugawanyika n.k ni miongoni mwa vitu vinavyoweka kibarua cha Ole kwenye wakati mgumu.
Hali sio shwari ndani ya United, vipigo dhidi ya Liverpool na Man City ndani ya Old Trafford vinaongeza vuguvugu la kumuondoa Ole klabuni hapo.
Mpaka sasa hali ilivyo ni kwamba, bodi ya wakurugenzi wa Man United na familia ya Glazers, hawana mpango wa kumfukuza Ole Gunnar Solskjaer muda wowote ujao. Kimsingi, suala hili – HALIPO!
Kwa lugha nyepesi, Ole Gunnar Solskjaer – Mitatu Tena!
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?


