Golikipa fundi wa Manchester United, David de Gea anasema kuwa anaamini wana kikosi bora kwa sasa ambacho kitawafanya wajikusanyie mataji. Amezungumzia changamoto iliyopo kuelekea kuwakabili PSG kwenye Ligi ya Mabingwa huku akisema -Hii ndiyo timu ya Manchester United na Tutashinda mataji.
Kwa mujibu wa De Gea, yeye na wachezaji wenzake wanajiandaa na wanawachukulia PSG kama changamoto inayowapa msukumo zaidi kwenye ligi hiyo ya mabingwa. Jumanne, Februari 12 watabe hawa wanamenyana na PSG.
Nyota huyu ameripotiwa kuwa yupo mbioni kusaini mkataba mwingine wa mda mrefu klabuni hapo. De Gea anawataja wanatimu wenzake Paul Pogba na Anthony Martial kama wachezaji waliorudisha tumaini jipya klabuni hapo huku wakiwa wanafukuzia vikombe; Kombe la FA, Ligi ya Mabingwa, na Ligi Kuu.
Golikipa huyu anaaminio kwa kikosi chao cha sasa ndani ya miezi mitatu ijayo watakuwa wanajivunia matunda ya jitihada zao.
“Tuna kikosi cha kushinda” -De Gea


Gabriel
Habar njema