Miongoni mwa tuzo zenye heshima barani Ulaya ni kiatu cha dhahabu ambacho hutolewa kwa mfungaji anayeongoza kwa kupachika mabao mengi kwenye ligi anayoichezea na kuonesha mchango mkubwa katika klabu yake. Kiatu hicho kilianza kutolewa tangu mwaka 1967/1968 ikiwa ni sehemu ya kutambua heshima na nafasi ya mchezaji aliyefanya vizuri ndani ya msimu husika.
Lionel Messi (Barcelona)
Anapewa nafasi kubwa ya kuibuka na tuzo hiyo baada ya kuwa na mwanzo mzuri wa ligi kwa msimu huu. Hadi sasa anaongoza kwa kuwa na magoli 21 ndani ya ligi hiyo huku akiwa amecheza mechi 20 za La Liga msimu huu. Mbali na hilo ametoa pasi zipatazo 10 za magoli ambazo zimewafanya wengine waweze kufunga. Messi ni aina ya wachezaji ambao wanafanya vyema sana kwa kufunga pia kuweza kuuchezea mipira kwa namna moja au nyingine.
Kylian Mbappe (PSG)
Ni hatua kubwa sana na ya muhimu kwa mchezaji huyu, ambaye kwa umri wake amefanya makubwa ambayo sio ya kubeza. Alianza kuwika alipokuwa na Monaco 2016/17 hadi kuwashawishi PSG kuvunja kibubu na kumvizia ili waweze kufanya naye kazi kwa kipindi chote hiki. Mbappe amevunja rekodi za kutosha hadi sasa kwa kuweza kushinda kombe la dunia akiwa na timu yake ya taifa, pia kuwania tuzo kubwa ya Ballon d’Or na jingine ni kufikisha idadi kubwa ya magoli kabla ya kufikisha umri wa miaka 21.
Cristiano Ronaldo (Juventus)
Hakuna neno linaweza kuelezea ubora wa mchezaji huyu kwa kipindi kilichopo na kijacho kutokana na kuvunja kila rekodi ambayo iliwahi kuwekwa ndani ya Madrid na nje ya klabu hiyo. Pia, ameweza kuweka rekodi ambazo haziwezi kuvunjwa na vizazi vya hivi karibuni ndani ya soka. Naye pamoja na umri wake kusogea lakini bado anaonekana kuwa katika kinyang’anyiro cha kuwania kiatu cha dhahabu. Hadi sasa katika ligi hiyo ana magoli 17 tayari. Swali la kujiuliza ni kwamba ataweza kuchukua hicho kiatu? Akiwa na klabu yake hiyo mpya?
Fabio Quagliarella (Sampdoria)
Sio klabu maarufu sana katika soka la hivi usoni lakini ni klabu ya muda mrefu sana na yenye heshima pia. Pamoja na umri wake kuwa umeenda lakini hajasahau nyavu ziko wapi, amekuwa na msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho kwa kufunga magoli 16 hadi sasa akiwa anamfukuzia Ronaldo. Bado anaendeleza ufundi wake aliokuwa nao ndani ya Juventus, Fiorentina na Napoli kabla ya kuhamia alipo kwa sasa. Kwa sasa ana rekodi ya kufunga katika mechi zake 11 za Serie A mfululizo akiifikia rekodi iliyowahi kuwekwa na mkongwe Batistuta.


Povel tz
Gud newa