Hazard amerudi juu tena kwenye vichwa vya habari kwa mara nyingine baada ya kuonekana kwamba amekwishaonja maisha ya klabuni hapo na sasa anaonekana kutaka kutimka klabuni hapo akajaribu maisha mengine pamoja na kuwaambia mashabiki wa klabu hiyo kwamba yeye anapenda maisha ya klabuni hapo. Lakini dalili za awali zinaonesha kabisa morali yake kuendelea kusalia hapo imeshuka kwa sasa.
Tangu alipoudhihirishia ulimwengu ubora wake duniani, Hazard amekuwa akihusishwa mara kwa mara kujiunga na Madrid ambao walionesha nia ya wazi kabisa ya kutaka kumsajili kikosini kwao ikiwa ni harakati zao za kufumua kikosi chao cha awali na kujenga kikosi kipya kitakachokuwa na ushindani zaidi ya hicho kilichopo sasa.
Hakuna kauli thabiti
Pamoja na kwamba yeye mwenyewe hajatoa kauli yoyote ile juu ya kuhama klabuni hapo lakini mashabiki wa klabu hiyo wameweza kuanza kujipa majibu na kuona kwamba mchezaji wao huyo hawezi kusalia zaidi ya msimu mmoja klabuni hapo kutokana na fununu zilizojengwa kwa kipindi kirefu na aina ya klabu ambayo inamhitaji kwa kipindi kirefu.
Kuchezea klabu kubwa huwa ni ndoto ya kila mchezaji na inapotokea wanapata nafasi wengi wao hawawezi kukataa nafasi hiyo ambayo huonekana kuwa na maslahi makubwa na kuwafanya wao kuuza zaidi na kuonekana zaidi kuwa ni wachezaji bora wanaotakiwa kupewa heshima ya namna fulani kwenye klabu zao.
Akiwa amewafungia Chelsea magoli 15 na kuchangia upatikanaji wa mengine 10, pia mkataba wa nyota huyo unaonekana kabisa kuelekea ukingoni huku kukionekana kabisa hakuna mazungumzo ya msingi yanayoendelea juu ya mchezaji huyo kuongeza kandarasi nyingine ili kuendelea kusalia Darajani hapo.
Wakimuuza itakuwaje?
Kumuuza mchezaji huyo kutawapa Chelsea kiwango kikubwa cha hela kisichopungua £100M, na kutokana na mmiliki wa klabu hiyo kuwa ni mtu anayeijua biashara lazima atawekeza kiwango hicho cha hela kwa kuangalia mbadala wa nyota huyo ili kuziba nafasi yake: japo sio rahisi kuziba nafasi ya mtu kwa namna moja au nyingine. Baadhi ya watu wanaoweza kutua kikosini hapo wameanza kuhusishwa akiwemo Hirving Lozano raia wa Mexico kutoka PSV.
Pia, wanaonesha kumvizia mchezaji wa Napoli, Lorenzo Insigne ili aweze kutua kikosini kwao endapo mchezaji wao atatimka kwa kipindi hicho. Mbali na hiyo tayari wameweza kumnyaka Pulisic kutoka Dortmund ambaye kwa namna moja au nyingine atakuwa msaada ndani ya kikosi chao kwa wakati ujao.
Mbali na hao tayari wanao nyota ambao wameweza kuwakuza wao wenyewe ndani ya kikosi chao ambao wanatazamiwa kuwa msaada hapo mbeleni kwenye kikosi hicho akiwepo Callum Hudson-Odoi ambaye anafananishwa uchezaji wake na Hazard. Hivyo, bado klabu itakuwa na uwezo wa kuwa na kikosi kipana sana.


Johnmary joel
Maamuzi yote tumuachie yy hazard#meridianbettz
Issa
Aondoke tu kwanza ajafanya maajabu
Povel
Haondoke tu mbadala hatapatiakana club kubwa kuliko mchezaj
Lydia Emmanuel Magoti
Kama mamuzi yake yatamruhusukuondoka aondoke tuu