Baada ya kupokea zawadi ya mkono wa magoli katika mechi yao ya awali ambayo wekundu hao walicheza soka la hovyo kuwahi kulicheza katika historia yao ya soka kwa kati ya misimu miwili ya hapa karibuni sasa Simba wamefufua matumaini upya baada ya kuwagomea Waarabu kuchukua alama mikononi mwao walipowakaribisha Waarabu uwanja wa taifa na kuwashikilia vilivyo kwa kuhakikisha wanajutia kutua katika ardhi hii bila kuondoka na alama ya aina yoyote ile.
Na hakika wameweza kufanikiwa katika hilo.
Mchezo ulikuwaje?
Alikuwa ni mshambuliaji hatari, John Bocco aliyeiona nafasi ya wazi kwa kumpa mchezaji mwenzake na mshambuliaji matata wa timu hiyo, Meddie Kagere mpira uliomfanya aweze kuwapa uongozi timu yake katika kipindi cha pili cha mchezo huo. Goli hilo pekee la Kagere limeweza kufufua matumaini kwa kikosi hicho japo bado hadi sasa wanafikiri juu ya kuwaombea njaa Vita Club na JS Saoura waweze kupoteza alama zao katika mechi zao ili yeye aendelee kupata nafasi zaidi ya kusonga mbele.
Msimamo
Kwa sasa Simba wapo nafasi ya pili katika msimamo wa kundi lao wakiwa na alama sita nyuma ya Al Ahly wanaoongoza kundi hilo wakiwa na alama saba kileleni. Na wapinzani wa Simba wanapishana kwa alama moja na mbili kitu ambacho kwa namna moja au nyingine bado kinawezekana endapo wao wataanza kwa kuwafunga wapinzani watakaocheza nao ndani na nje ya viwanja vyake vya nyumbani.
Bado wana shughuli pevu katika kundi lao kutokana na uwiano wa alama ambao kila mmoja anao na kuangalia mahitaji ambayo kila mmoja anayahitaji ili kuweza kupata nafasi ambayo itawapa uhakika wa kuendelea kukaa katika nafasi hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa itawafanya waweze kuweka historia iliyopotea kwa kipindi kirefu.
Kwa namna michuano hii inavyokwenda hasa katika hatua hiyo ya makundi sio rahisi kutabiri nani anaweza kuibuka nafasi ya juu kutokana na kila klabu kuonekana ipo kwenye ushindani mkubwa sana ambao unamfanya kila mmoja ajiandae kuipa heshima klabu yake na kuweka heshima ndani ya vilabu vyao na kulipa fadhila kwa mashabiki zao.
Tutegemee nini?
Tuwape nafasi zaidi ndani ya michuano hiyo pamoja na ugumu uliopo katika michuano hiyo, hata wakikosa nafasi hiyo wataweza kujiandaa zaidi kwenye michuano ijayo ambayo watakuwa wamepata na kujenga uzoefu zaidi baada ya kuwa nje ya michuano kwa kipindi kirefu sana na watakuwa wamefika hatua nzuri sana kwa aina ya timu alizokutana nazo maana zina uzoefu wa muda mrefu.


Povel
Simba baba lao