Kila klabu duniani huwa na aina ya wachezaji ambao hushikilia rekodi fulani ambayo huwa imeisaidia klabu hiyo kuwa katika hatua fulani kisoka. Baadhi ya klabu kubwa huwa na watu ambao hutuzwa kama mifano kwa wachezaji wengine kufuata nyayo zao pale inapobidi. Klabu ya Barcelona ina historia kubwa sana ambayo sio rahisi kupotea. Baadhi ya wachezaji waliochangia kujenga historia hiyo klabuni Barca ni hawa:
Lionel Messi
Sio jambo la kushangaza kumwona Messi katika nafasi hii, akiwa amechangia kwa kiwango kikubwa kufunga idadi kubwa ya magoli ndani ya kikosi hicho na kujenga historia na heshima kubwa hadi kuingia katika vitabu vya kihistoria vya klabu hiyo. Ameweza kuifungia klabu hiyo magoli 577 katika mechi zake 661 alizozicheza. Na bado historia hiyo inaendelea kwa sababu bado hajastaafu kucheza soka hilo hivyo kuna uwezekano wa kuvunja rekodi nyingi zaidi ndani ya kikosi hicho.
Cesar Rodriguez
Baada ya kushikilia nafasi hiyo kwa kipindi kirefu sana amekuja kuachia kipindi cha hivi karibuni baada ya Messi kuzifikia takwinu zake. Japo kila mmoja anabaki na heshima yake ndani ya klabu hiyo. Aliweza kuwafungia Barcelona magoli 232 katika mechi 351 alizocheza chini ya klabu hiyo yenye historia ya pekee. Amechangia katika makombe matano ya ligi yaliyo kwenye stoo za klabu hiyo hadi leo.
Laszlo Kubala
Alijiunga na klabu hiyo miaka ya 1950 na kuweka historia ambayo ilidumu kwa kipindi kirefu na kuifanya klabu hiyo kukaa kwenye vitabu vya historia hadi leo. Na rekodi yake imekaa kipindi kirefu sana hadi kuja kuvunjwa. AliwafungiaBarcelona magoli 194 ambayo yalikuwa ya kihistoria ndani ya kikosi hicho.
Josep Samitier
Miaka ile waliweza kumpa jina la utani kama ‘The Grasshopper’ kutokana na uwezo wake aliokuwa nao ndani ya eneo la mpinzani wake. Anakumbukwa miaka yake ya 1932 alipoonesha maamuzi yake magumu na kutoka kwa mahasimu wao Real Madrid hadi kujiunga na klabu hiyo. Mashabiki wengi wa klabu hiyo walimkasirikia kutokana na hilo. Pamoja na hayo anaingia kwenye vitabu vya kihistoria kwa kufunga magoli 184 ndani ya klabu hiyo.
Hao ni sehemu tu ya historia ya klabu hiyo ambao kwa nafasi moja au nyingine wamechangia katika kuijenga klabu hiyo na kuifanya ifahamike na kuwa tishio sana duniani hadi leo. Wachezaji wengi wa kileo wanaishi na kufanya mambo yao kwa falsafa za wakongwe hawa.


isha
Hongera sana barcelona
Furahav
Safi.