Meneja wa sasa wa Chelsea Maurizio Sarri anaonekana ameshapoteza radha pale klabuni Chelsea kukiwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya wadau na mashabiki kuwa meneja huyu atimuliwe tu! Taarifa zinadai Chelsea wanamtaka aliyekuwa meneja wa Real Madrid Zinedine zidane kuchukua nafasi klabuni hapo kabla ya kumng’oa Maurizio Sarri.
Zidane kwa mda kidogo amekuwa nje ya majukumu ya kiutawala tokea alipoaamua kuachia kibarua pale Real Madrid kama meneja. Zidane ambaye ana umri wa miaka 46 amepata mafanikio makubwa akiwa Real Madrid, ameshinda Ligi ya Mabingwa mara 3 mfululizo.!
Sarri amekuwa akikosolewa siku za hivi karibuni kufuiatia matokeo yasiyoridhisha ya The Blues. Kichapo walichokipata cha bao 6-0 dhidi ya Manchester City kimeongeza msikumo zaidi kwa wadau wa klabu hii kuona kama meneja huyu sasa anahitaji kuwaachia klabu yao.

Kwa mujibu wa The Sun, klabu ya Chelsea inataka Zidane achukue nafasi hiyo haraka iwezekanavyo. Hata hivyo, muwakilishi wa Zidane anasema kuwa Zidane aliamua kutumia msimu huu wote bila kujihusisha na klabu yeyote kabla hajaamua kurejea rasmi, hii inaleta mashaka kwa klabu hii kumnasa.
Hata hivyo, Chelsea wanakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka klabu ya Manchester United ambao pia wanahusishwa zaidi na Zinedine Zidane. Man united wanadaiwa bado wapo mawindoni wakati Ole Gunnar akionesha kuanza vizuri kwa kutoshindwa kwenye gemu zake 11 kabla hajapokea kichapo cha 2-0 Jumanne.


Povel
Gud news