Namba 4 za Ed Woodward

Baada ya kipindi cha fungate cha kocha wa mpito wa United, Ole Gunnar Solskjaer kuisha kutokana na kupokea kichapo kutoka kwa mabingwa wa Ufaransa PSG katika hatua ya 16 bora Champions League sasa wana jukumu zito la kuangalia namna gani wanaweza kujitahidi kufanya kila linalowezekana kuweza kusonga mbele zaidi katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.

Pamoja na matokeo hayo bado wanaangalia namna watakavyoweza kupata mwakilishi wa kudumu kuweza kukishika kikosi hicho kwa wakati wote uliosalia. Tunaweza kusema Ole ameanza maisha rasmi ndani ya klabu hiyo tangu apewe kibarua hicho cha kuinoa timu hiyo ambayo inaonekana kurejea kwenye uimara wake.

Kwa hali ya kikosi ilivyo na aina ya mechi zilivyo kwa kipindi hiki kwa kuonekana kila klabu imejizatiti kujenga heshima; United wanatakiwa kufanya usajili mkubwa sana ili kukijenga upya kikosi chao kiweze kuwa katika ushindani mkubwa ambao kikosi hicho kiliwahi kuwa nao miaka ya nyuma.

Katika hatua ya kuimarisha kikosi hicho, Ed Woodward ameanza kurusha jicho lake kwa baadhi ya wachezaji ambao anaona watafaa kujenga kikosi anachoona kitafaa zaidi kuleta ushindani hapo baadaye na katika michuano yote ambayo klabu hiyo itakabiliana nayo kwa siku za usoni na baadaye. Na kwa mahitaji ya sasa anajua kabisa kwamba kikosi hicho kinahitaji mlinzi wa kati, walinzi wa pembeni na viungo ili kuwapunguzia majukumu baadhi ya wachezaji.

Katika safu ya ulinzi wamebaki kurusha jicho lao kwa mchezaji wa Napoli waliyeanza kushughulika naye tangia dirisha dogo, Kalidou Koulibaly ambapo klabu hiyo imeonekana kuhitaji kitita cha £90M ili kufanya biashara na United wanaoonesha nia ya kumsajili nyota huyo raia wa Senegal.

Mbali na mchezaji huyo pia wanamfuatilia nyota wa Atletico, Lucas Hernandez kutokana na uwezo wake wa kumudu kucheza upande wa kulia au kushoto katika safu ya ulinzi na hilo ndilo ambalo klabu hiyo inatamani na inapenda litokee kwa sababu atakidhi mahitaji ya kikosi chao.

Upande wa kulia wanamfukuzia Nikola Milenkovic mchezaji wa Fiorentina ambaye wanahisi anaweza kuwa mbadala wa Valencia hapo baadaye kutokana na umri wake kusogea. Na eneo la mwisho ni Douglas Costa ambaye walihusishwa naye hata kwa kipindi cha nyuma kwanba angejiunga nao.

Jambo hili linasubiri kwanza kujua hatma ya nani atapewa mikoba ya kukinoa kikosi hicho kwa mkataba. Jumatatu hii Ole atakuwa na kibarua kingine kudhihirisha ubora wake mbele ya Chelsea katika michuano ya FA ambapo kushinda kwake kutakuwa kunaendelea kumjengea wasifu kuelekea kupigania nafasi ya kupewa mkataba wa moja kwa moja wanaochuana na Mauricio.

3 Komentara

    Gud news

    Jibu

    Habari nzuri

    Jibu

    Mtu mbaya

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.