Hatua Kubwa Aliyopiga Shaqiri

Nyota wa Liverpool Xhedran Shaqiri amewathibitishia kuwa yeye siyo mtu wa mchezo mchezo wale waliokuwa wanadhani ataenda kuboronga klabuni Liverpool. Shaqiri amepiga hatua kubwa tangia alipoingia klabuni hapo.

Msimu huu nyota huyu amekuwa mmoja wa wachezaji tegemezi pale inapohitajika kuokoa Jahazi kwenye kikosi cha Jurgen Klopp, ambao kwa sasa wanakimbizana na Manchester City kwenye kilele cha Ligi ya Uingereza.

Shaqiri mwenye miaka 27 amechapa magoli 6 kwenye gemu 20 alizowachezea vinara hawo msimu huu, akiwa ni mmoja wa waliomfukuzisha kazi Jose Mourinho baada ya kucheka na nyavu mara 2 kwenye gemu waliyoshinda bao 3-1 dhidi ya Man U.

Kuna wasiwasi kama nyota huyu atacheza gemu inayofuata ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi yake ya zamani ya Bayern Munich Jumanne hii.

Shaqiri aliingia klabuni hapo akitokea kule Stock City ambayo kwa wakati huo ilishuka daraja kutoka kwenye Ligi Kuu msimu uliopita kwa ada inayotajwa kuwa paundi milioni 13.5.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.