Nigeria: Ambao Hawajawahi Kucheza Huko

Nigeria ni miongoni mwa nchi zinazoheshimika duniani hasa upande wa soka. Ina wachezaji wengi wenye vipaji na uwezo mkubwa sana. Pamoja na hilo kuna wachezaji ambao hawajawahi kugusa majina yao katika kikosi cha Super Eagles ambacho mara nyingi huwa tishio sana kwenye michuano mbalimbali. Kuna baadhi ya wachezaji pamoja na ubora wao hawajawahi bahatika kuwa sehemu ya kikosi hicho.

Chuba Akpom

Nyota huyo mwenye asili ya Nigeria anaiwakilisha Uingereza katika michuano mbalimbali pamoja na kuwa taifa lake mama ni Nigeria na ana kila sababu ya kuligeukia kwa upande wa pili taifa lake kwa nafasi yake na kulichezea. Kwa sasa anakipiga katika klabu ya Brighton and Hove Albion.

Sidney Sam

Mchezaji huyo anayekipiga katika taifa la Ujerumani alilikataa taifa lake la Nigeria kwa kinywa chake na kuona hana chochote kuweza kujiita yeye kama raia wa taifa hilo; ndipo akaamua kujiunga na upande wa pili wa Wajerumani ili afanye makubwa zaidi huko. Kwa sasa anaichezea SV Darmstadt 98.

Dele Alli

Mnigeria lakini ameishi maisha yake yote Uingereza. Kwa sasa anaichezea Tottenham na ni miongoni mwa mazao yanayochipukia kwenye soka kwa wakati uliopo kutokana na uwezo wao unaoonekana na matokeo yanayodhihirika wazi kabisa. Ni kizazi ambacho kingekuwa Afrika ingekuwa nafasi kubwa sana kuwika kimichezo.

Ross Barkley

Alipelekwa Uungereza na babu yake ambako kwa kiasi fulani amekulia huko na baadaye kuzama katika soka ambako alifanikiwa kuichezea timu ya taifa hilo baada ya kuitwa kikosini. Kwa sasa anacheza katika klabu ya Chelsea kama kiungo wa timu hiyo.

David Olatokunbo Alaba

Jina lake tu linasadifu kwamba mchezaji huyo ni raia wa taifa hilo la Nigeria aliyefanikiwa kucheza soka la ughaibuni na kuchukua uraia wa nchi hizo. Mchezaji huyo wa klabu ya Bayern Munich na kikosi cha timu ya taifa ya Austria kwa historia ni mchezaji halali wa Nigeria lakini harakati za maisha kifamilia zilimfanya kulihama taifa hilo.

Kiuhalisia Nigeria ni kisiwa cha vipaji kutokana na aina ya majina ya wachezaji waliochimbukia ndani ya taifa hilo na kuchukua utaifa wa mataifa hayo waliyohamia. Kwa mazingira halisi endapo wangebaki katika taifa lao kikosi chao kingekuwa tishio; kwa sababu hawa ni baadhi tu.

3 Komentara

    Mmh sio poa.

    Jibu

    Hapo mwendo wa ushnd tu hapo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.