Wenye Utajiri Mkubwa…

Wachezaji wengi wenye utajiri mkubwa duniani huupata kutokana na mikataba yao inayowajali na kuwafanya kuwa huru kufanya mambo mengi bila kuwa na mipaka; vilevile baadhi ya tuzo na nyongeza mbalimbali ndani ya mishahara yao na mikataba ya nje ya wadhamini mbalimbali wanaowiwa kufanya uwekezaji wa matangazo kwa wachezaji wa aina yake. Baadhi ya wachezaji wanaoshikilia pesa ndefu kwa sasa ni kama vile:

Cristiano Ronaldo

Utajiri wa Ronaldo unakadiriwa kuwa ni $450M kwa sasa na mapato yake yanatanuka mara kwa mara kutokana na mshahara wake ambao unafanya aweze kujaza kapu lake kadri siku zinavyozidi sogea mbele. Na mshahara wake unafika kiasi cha $61M ambacho sio kiasi cha mchezo kwa mchezaji kulipwa.

Lionel Messi

Kwa mshahara anaoupokea mchezaji huyo ilibidi azidi mapato ya Ronaldo kwa kiasi fulani kwa sababu anapokea mshahara mzito zaidi yake; mshahara ambao ni zaidi ya $84M kitu ambacho ni mbali sana na kile cha mpinzani wake Ronaldo. Lakini utajiri wake unasomeka $400M, kiwango hicho ni pamoja na mikataba ya kibiashara; hivyo alipaswa kuwa juu kabisa ya mwenzake.

Zlatan Ibrahimovic

Ni mchezaji mkongwe sana katika soka ambaye ameweka historia kubwa sana na anaendelea kufanya hivyo pamoja na umri wake kusonga mbele kidogo. Mbali na kuwa na vitegauchumi vinavyomfanya kuwa bora kiuchumi; pia ameweza kucheza katika vilabu vikubwa ikiwemo Juventus, Barcelona na Manchester United.

Wayne Rooney

Mchezaji wa Uingereza aliyestaafu kuichezea timu yake ya taifa kwa sasa. Anakadiriwa kuwa na utajiri wa $145M ambao ameupata katika maisha yake ya soka hadi sasa akiwa bado anacheza soka kule Marekani. Mchezaji huyo wa zamani wa United amekuwa mchezaji wa Kiingereza aliyefikia hatua kubwa sana kwenye soka kitu ambacho wachezaji wengi wanakitamani na heshima hiyo wanaitamani.

Neymar

Mchezaji huyo wa PSG, kutokana na takwimu za Forbes, anamzidi kwa kiasi fulani kimauzo Ronaldo lakini utajiri wake bado upo chini na unakadiriwa kuwa ni $140M. Utajiri wake anautengeneza kutokana na mikataba ya mauzo kibiashara na Nike pia na Dre Beats. Mbali na wachezaji hao pia wapo wengine kama Luis Suarez, Sergio Arguero.

5 Komentara

    Kweli kabisa pongezi kwao

    Jibu

    Asante kwa habari#meridianbettz

    Jibu

    Hongera azao

    Jibu

    Wanatisha

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.