Klabu ya Chelsea imekuwa ikipata matokeo mchanganyiko siku za hivi karibuni huku kutoridisha kwa matokeo kukichukua nafasi kubwa. Sarri amekuwa akishikiwa kidedea na baadhi ya mashabiki kuwa asepe klabuni hapo, lakini utawala wa klabu hiyo unadaiwa kuwa unampa mda zaidi wa matazamio. Inakuwaje tena anahusishwa na kwenda klabu ya Roma!
Mashabiki wenye utani walisitiza kuwa ni bora meneja huyo akaenda kuvuta sigara huko akaachana na klabu yao. Hata hivyo, wakati maneno hayo yakipamba moto kwenye mitandao stori zingine zimekuwa zikimtaja meneja huyu akihusiana na klabu ya Roma, kama ni kweli basi huenda wanajaribu kumnasa ajiunge na klabu hiyo baada ya mkataba wakje kuisha.
Japokuwa meneja huyu alisema kuwa hana wasiwasi kuhusu hatma yake klabuni hapo, ni wazi kuwa kama akitimuliwa basi atahitaji kupata timu nyingine, bila shaka nafasi hiyo inaweza kuwa imembamba wakati muafaka kabisa.
Anachokisema yeye
Meneja huyu baada ya kikosi chake kutwaa ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Malmo sasa, anaamini kikosi chake kinaweza kurekebisha makosa na hatimaye kupata ushindi zaidi na kurekebisha hali ya hewa klabuni hapo.
Sarri pia amekanusha fununu za kuhusishwa kwake na klabu ya Roma, anadai kuwa bado ana mkataba na Chelsea kwa msimu ujao kwa hiyo yeye kwenda Roma haiwezekani.
Chelsea wanakibarua kingine kwenye gemu fainali ya Carabao Cup dhidi ya Man City Jumapili hii. Kila upande unatarajia kulichukua taji hili.


Furahav
Kweli ukocha kazi sana.
Povel tz
Habar njema
Ally mohamedi ally
Habar njema