Manchester United wanakabiriwa na moja ya gemu ngumu na muhimu ili waendelee kupambania nafasi yao ya kumaliza katika 4 bora kama ili waweze kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya. Anthony Martial na Jesse Lingard wanaripotiwa kuwa huwenda wakatimba dimbani kuwavaa Liverpool.
Meneja wa klabu hiyo Ole Gunnar ana matumaini kuwa vijana wake hao watarejea dimbani baada ya kutoka kuuguza majeraha yao, hivyo bila shaka jumapili wanaweza kuwepo dimbani kuongeza chchu ya ushindi.
Lingard mwenye miaka 26 shida ya msuli kwenye gemu dhidi ya PSG na alitarajiwa kuwepo nje ya dimba kwa mda wa wiki karibia tatu.
Anthony Martial pia alipata jeraha kwenye kipindi cha kwanza cha gemu hiyo hiyo dhidi ya PSG. naye anatarajiwa kuwa sawa kuelekea kwenye gemu dhidi ya Liverpool.
“Jesse anaonekana yupo poa, natumaini na Anthony pia.” -Solskajaer
Ole Gunnar anaamini kwa mda amabao umebakia kwa maandalizi kuelekea gemu hiyo wakali hawa watakuwa wamerejea wakiwa fiti kabisa.


isha
Hatari sana