Klabu ya Chelsea imepigwa nyundo ya kutokufanya usajili wowote kwa muda wa misimu miwili na Shirikisho la Soka la Dunia. Adhabu hiyo imekuja wakati klabu hiyo ikiwa katika kipindi cha kutaka kuimarisha kikosi chake ili kuweza kuondoa sintofahamu ya wao kupoteza mechi nyingi ndani ya ligi inayopendwa sana duniani.
Kwanini hukumu hii?
Sababu kubwa ya klabu hiyo kupigwa adhabu hiyo ni kutokana na kuvunja kanuni ya usajili wa vijana wanaojiunga na academy yao ambayo huwa na nia ya kuandaa kizazi cha baadaye ndani ya soka la nchi husika na duniani kwa ujumla. Sasa, klabu hiyo imejikuta ikishindwa kutumia vizuri mamlaka ya usajili waliyonayo chini ya FIFA na kuambulia kukutana na mkono wa hukumu kubwa.
Mbali na kufungiwa usajili ndani ya misimu miwili pia wametahadharishwa kufanya marekebisho ya haraka kwa makosa waliyoyafanya ili kuondoa pungufu hilo kubwa lililofanyika kwa wakati uliopo. Pamoja na adhabu hiyo pia wamepigwa faini ya £460,000 iweze kulipwa kutokana na kukiuka mikataba ya kimakubaliano na shirikisho hilo juu ya usajili.
Fahamu zaidi
Sababu kubwa ya adhabu hiyo ni kusajili vijana ambao hawajafikia umri ambao shirikisho hilo huhitaji, ambapo kwa wanaofikisha umri huo huruhusiwa kutoa huduma za kimichezo katika klabu husika. Mbali na hilo; klabu hiyo imeanza hatua za kukata rufaa kupinga maamuzi hayo mazito yenye nia ya kuonekana kudhoofisha uwezo wa kikosi hicho.
Adhabu hiyo imekuja wakati ambao Maurizio Sarri anahangaika kuleta utulivu ndani ya kikosi hicho cha Chelsea baada ya kuwa na msinu mbaya tofauti na hapo awali alivyokuwa anaanza kuonesha makali yake baada ya kupokea mikoba ya Conte. Anaona kama kila kinachofanywa kinaminya jitihada zake za kusonga mbele zaidi.
Hata baadaye yake ndani ya kikosi hicho imeingiwa na mashaka makubwa baada ya kupoteza mfululizo, pia kutokana na fununu zinazoendelea juu ya klabu hiyo kuonekana kuanza kunyemelea huduma za Steve Holland ambaye ni sehemu ya makocha katika timu ya taifa ya Uingereza; suala hili linaweza kuwa linamtesa pia mwalimu huyo kwa upande mwingine akilinganisha mafanikio ambayo hajayafikia kabisa ndani ya kikosi hicho chenye kiu ya mataji kwa kipindi kirefu.
Pamoja na hilo, Chelsea bado ina kikosi kipana ambacho wachezaji wqke wengi wapo nje kwa mkopo. Kwa sababu adhabu hiyo haiwazuii wao kuwarudisha wachezaji wao ambao wanacheza nje ya klabu hiyo kwa mkopo. Na wao wana utajiri mkubwa wa wachezaji wa aina hii ambao bado wanasakata kabumbu na wangeweza kurudi wakati wowote klabuni hapo. Hivyo, pamoja na hasara ambayo wataingia bado wana uwezo wa kuonesha ushindani kwani wana wachezaji wengi; pia wana ingizo jipya akiwemo Pulisic ambaye msimu ujao atakuwa ndani ya klabu hiyo.


Povel
Duh majanga sana
Furahav
Hatari sana.
Issa
Ni safi kwake