Tottenham wameendelea na majanga ya kupokea vipigo hivi karibuni baada ya kuoneshwa kazi ngumu na Chelsea ambao walimchezea mchezo ambao uliwafanya wapotee kabisa mchezoni na kuonekana kama hawapo kabisa mchezoni kwa wakati ule. Hali hiyo inawafanya mashabiki wao waanze kupoteza imani kiasi na timu yao.
Wakati hali ikiwa hivyo ni haohao Tottenham wanajiandaa kucheza mechi yao na Washika Bunduki wa Uingereza, Arsenal katika uwanja wao wa nyumbani; mechi inayoonekana kuwa ngumu kabisa miongoni mwa pande zote mbili kutokana na hali kwamba kila mmoja anauhitaji mkubwa wa alama tatu ili kuweza kujithibitishia kwamba nafasi ya kileleni ni yake la sivyo atakuwa anatengeneza mazingira kwa wengine kushika nafasi hiyo.
Mbali na hilo Spurs wana idadi kubwa ya wachezaji ambao uwezo wao haubezwi pindi wakiwa katika majukumu ya kutafuta alama ambazo zitawasaidia wao kumaliza wakiwa nafasi za juu. Lakini kuna baadhi ya wachezaji ambao kwa upande mwingine wanaonekana kama hawana kile ambacho mashabiki wao walitegemea kukiona kwao. Baadhi yao ni:
Hugo Lloris
Pamoja na kuutwaa ubingwa wa kombe la dunia na kupewa heshima ya kuwa mlinda mlango namba moja nchini kwao lakini pia ameendelea katika hali hiyo ya kuwa chaguo la kwanza hata katika klabu yake. Kwa heshima anayopewa amekuwa akifanya makosa ya makusudi mara nyingi ambayo yamekuwa yakiigharimu timu yake kwa kukosa mawasiliano mazuri na safu yake ya ulinzi. Tatizo hili linaonekana kumtafuna kocha huyo kikosini.
Kieran Trippier
Anakumbukwa sana kwa kile alichokifanya wakati wa kombe la dunia wakiwa wanacheza na Croatia kutokana na mpira alioucheza na kuipa timu yake matokeo mazuri. Lakini pia ni miongoni mwa walinzi ambao wanafanya kazi nzuri sana uwanjani, kitu ambacho kinaonekana kuwa tatizo kwake kikosini hapo ni kukosa umakini pindi anapokuwa anatekeleza majukumu yake uwanjani na hivyo kugharimu sana timu yake.
Serge Aurier
Mchezaji huyu ni mbadala wa Trippier katika namba yake jambo ambalo linaonekana kuwaumiza mashabiki ni wachezaji wote wawili kukosa nidhamu ya kimchezo wakiwa kwenye majukumu hayo. Wanaona ni vema wamkose Serge kuliko akiwepo pamoja na kwamba wawili hawa wamekuwa na mapungufu yanayozidiana katika upande wao. Uwepo wake mara nyingi hauwapi imani ya ushindi mashabiki wao kwa kukosa kabisa kumuamini kama anamudu kuwapa matokeo chanya.
Tutegemee kuona Pochettino akirekebisha makosa hayo leo kikosini.


Furahav
Noma sana.
Mariam mtandama
Safi
Caroline
Dah atari
Lydia Emmanuel Magoti
Duu atarii
Zeiyana
Tottenham mnatuangusha mashabiki wenu
Povel
Habar njema