Kumekuwa na stori kibao kuhusu hatma ya Mauro Icardi klabuni Inter Milan na kuhushwa kwake na vilabu mbalimbali. Mkewe Icardi Wanda Nara ambaye pia ni wakala wa mchezaji huyo ameonekana kuwa na mchango mkubwa zaidi katika hali inayoendelea juu ya uhusiano wa nyota huyu na klabu yake.
Antonio Cassano mara ya kwanza Antonio Cassano alimshambulia mwanamama huyo kuwa ndiye sababu ya mmewe kuvuliwa ukapteni klabuni hapo. Cassano alizungumza kwenye kipindi cha Tiki Taka, na hajataka kupepesa macho kuzungumza tena tuhuma zake mbele yake.
Staa huyu wa zamani, ambaye anaiita hali inayoendelea juu ya uhusiano wa Icardi na Klabu yake kuwa ni janga anasisitiza kuwa ni janga ambalo limetengenezwa na Nara, amemshauri Nara amwambie mmewe aombe msamaha kwa wanatimu wenzake kabla hali ya hewa haijawa mbaya zaidi.
Cassano anasema kuwa tatizo la mke wa Icardi ni kuwa anaongea sana na anatumia vibaya mitandao ya kijamii. Bwana huyu amesisitiza kuwa kuvuliwa kwa unahodha kwa Icardi kusingetokea bila sababu kwa kuwa Ausilo, Marotta, Spalletti na Zhang sio vichaa isipokuwa mwanamama huyu anatumia mitandao vibaya kumharibia mme wake.


Warda
Icardi mwenyew mpole sana #Meridianbettz
Caroline
Ukiwa star shida kweli
Furahav
Hatari sana.
Povel
Habar njema
Zeiyana
Ukiwa star kazi kubwa