Nje Ndani za Madrid

Madrid wamepoteza mechi yao ya pili mfululizo mbele ya Barcelona ambao wamekuwa kwenye msimu mzuri sana kwa sasa. Mechi hizo zote mbili wamezipoteza wakiwa nyumbani kwao ambapo mechi ya kwanza ilikuwa ni ya Copa del Rey na kuwafanya kukaa nje ya kinyang’anyiro cha kuwania kombe hilo mbele ya miamba hao walio kwenye hali nzuri msimu huu.

Kutokana na matokeo hayo kuna hatari kubwa kwa Madrid kumaliza msimu bila kikombe chochote kwani hata nafasi yao ya ndani ya ligi kuna tofauti kubwa sana kati yake na kinara wa ligi hiyo ambaye ndiye alikutana naye. Pia, ameshindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani mara kadhaa katika mechi nyingi.

Mbali na hilo kwa sasa amebakiwa na nafasi moja ya kujaribu kuonesha makucha yake kama ataweza kurejesha heshima ambayo imetoweka kutokana na kupokea vichapo vingi vya ajabu mbele ya wapinzani wake. Kikombe anachokiangalia kwa sasa ni kile cha ligi ya mabingwa barani Ulaya ambako nako upinzani wake sio suala la mchezo kabisa; na anapewa nafasi ndogo sana kufanya vizuri kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Madrid

Mlinzi wa klabu hiyo Carvajal anaona kwa sasa kama mchezo wa soka haujawa na usawa kwao kutokana na kile wanachokumbana nacho ndani ya mechi yao. Maana imekuwa ni hali ambayo hata wao wanashindwa kabisa kuielewa kutokana na kile kinachoendelea ndani yao, wanapambana kupata matokeo lakini hawayapati vile wanavyoonelea wao ingekuwa.

Goli pekee la Raktic ndani ya mechi hiyo liliweza kuibua matatizo ndani ya kikosi hicho na kuwapa mwendelezo mbaya wa matokeo ambayo kwao msimu huu imekuwa ni kama tatizo sugu ambalo halina tiba. Japo sio wao wa kwanza kukutana na kasumba hiyo; inakumbukwa hata Barcelona msimu uliopita aliweza kuwa na tatizo kama hilo japo upande wa Madrid imekuwa ni zaidi.

Historia yawekwa na msimamo

Kutokana na matokeo hayo, Barcelona inakuwa klabu ya kwanza kushinda mechi zote tatu ndani ya Santiago Bernabeu ikiwa hakuna klabu ambayo iliwahi kuondoka na ushindi mara tatu mfululizo ndani uwanja huo wenye heshima kubwa sana kwenye soka. Kwa hali ya haraka sasa Madrid atakuwa nyuma kwa alama 12 katika ligi hiyo huku akiwa nafasi ya tatu.

Huku Barcelona wakiondoka na ushindi huo upande wao wanasifu aina ya matokeo waliyoyapata na nafasi yao nzuri kuelekea ubingwa ambao hadi sasa anaonekana kupigilia msumari mzito ambao sio rahisi kwa yeyote kuung’oa. Amejiweka katika nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa huo. Pia, ndani ya kikosi hicho, Samuel Umtiti anaendelea kusugua benchi mbele ya Lenglet ambaye anaonekana kuwa mlinzi mwenye kitu cha kipekee sana kwa sasa ndani ya kikosi chao; hivyo kwa sasa anapewa nafasi ndogo sana.

6 Komentara

    Ninavyoipenda Madrid ndivyo inajua kuniangusha #Meridianbettz

    Jibu

    Asanteni Kwa taarifa meridian

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Madrid ni noma

    Jibu

    Kujikwaa si kuanguka Real Madrid chama kubwa aliwezi kuanguka kiraisi hivyo

    Jibu

    madrid wapo vizuri sana

    Jibu

Acha ujumbe