Timu zimeanza kuweka mezani mipango ya kutumia pesa nyingi kuwabamba wachezaji wakali msimu huu unakuja wa joto. Manchester City kama klabu zingine nao kama kawaida wapo kwenye mpango wa kukipa nguvu zaidi kikosi kwa fungu la paundi 350m wakati wa usajili.
Kwa mujibu wa ripoti meneja Pep Guardiola anapanga kutumia kitita hicho cha pesa kuwanasa wachezaji wanne watakaoongeza moto klabuni hapo wakilenga beki wa kushoto na kiungo pia.
Mancity ambao kwa sasa wanafukuzia mataji manne kuelekea mwisho wa msimu wanasaka kuwa na kikosi bora zaidi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. “kuna nafasi tatu au nne hivi natakiwa kuziangazia lakini pia kuna mawazo ambayo tunayo” -Guardiola
Guardiola anadaiwa kuwa anamuangazia nyota wa Leicester Ben Chilwell baada ya kuona kuwa hataweza kumuamini Benjamini Mendy ambaye anaonekana kama hajakuwa na matokeo yale wanayoyategemea. Guardiola anafikiria mastaa wengine watakaoingia kwenye orodha ya kutumia kitita hicho.

