Mashetani wekundu wanadaiwa kuwa kwenye mpango kabambe wa kumwaga pesa kumnasa nyota wa Borussiaa Dortmund Jadon Sancho. Tetesi zinadai kuwa Man U wamekutana na kikwazo cha kumnasa nyota huyu anayeripotiwa kuwa na thamani ya paiundi milioni 100 baada ya wapinzani wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya PSG kuonekana nao wako sambamba na klabu hiyo kumfukuzia staa huyo.
Mabingwa gongana vichwa kwenye gemu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi uliopita huku Man U wakiambulia kichapo cha bao 2-0 ikiwa ni gemu ya kwanza kwa klabu hiyo kupoteza tokea walipompata Ole Gunnar kama meneja wao wa mda.
Kwa mujibu wa taarifda klabu hii wako tayari kutumia pesa kibao kuwahi kutumika na upande huo wa Premier League kumnasa mshambuliaji huyu kinda wa miaka 18 msimu unakuja wa Joto. Dau la paundi milioni 100 ni dau kubwa zaidi ya dau ambalo klabu hiyo ililipa kwa Paul Pogba kutoka Juventus mwaka 2016.
Hata hivyo mabingwa wa Ufaransa, PSG nao wanadaiwa kuwa wapo kwenye mbio hizohizo za kumnasa nyota huyu kijana. Wnataka staa huyu akaungane na vijana wengine kwenye safu ya ushambuliaji ya Kylian Mbappe na Neymar.


Chiku
Wako vizur