Klabu ya Azam imepata pigo kuelekea mchezo wa Ligi kuu ya NBC dhidi ya mabingwa watetezi Simba SC baada ya wachezaji wake watatu kujiunga na timu za taifa kwajili ya mashindano ya AFCON.

Nyota wa Azam walioitwa katika timu zao za taifa ni pamoja na Prince Dube aliyepona majeraha ya muda mrefu, Bruce Kangwa na Never Tigere waliojiunga na timu ya Taifa ya Zimbabwe.
“Kukosekana kwa wachezaji hao ni pigo kulingana na mchezo unaotukabili, hii inaweza kutugharimu. Lakini kocha anaangalia namna ya kuwatumia wale waliopo kuweza kufanya vizuri.”alisema msemaji wa Azam, Thabit Zakaria (Zaka za Kazi).
“Kocha anawaamini vijana waliopo na anajaribu kuwatumia na kujipanga na mchezo ujao kwaajili ya kupigani alama tatu.”aliongeza.
Wachezaji wengine watakao kosekana ni pamoja na Idd Seleman ‘Nado’, Ayoub Lyanga na Ivan Mbara kwasababu ya majeraha.
Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

CHEZA HAPA

