Tuanzebe Kutua Napoli Januari Hii.

Ama hakika maisha ni safari, Axel Tuanzebe ni mfano hai katika hili. Amekuwa na safari za kuingia na kutoka Man United. Italia kunamsubiri.

Tuanzebe ni miongoni mwa wachezaji waliokuzwa ndani ya akademi ya Manchester United. Ni dhahiri, idadi ya wachezaji katika idara ya ulinzi pale United ni kubwa ikiwa ni sambamba na ubora wao viwanjani.

Axel amekuwa akipata namba kwa tabu kwenye kikosi cha United. Aling’ara na kupata sifa kemkem alivyoisaidia Aston Villa kupanda ligi kuu na baadae alirejea United. Maisha ndani ya United yakaendelea kuwa kama alivyoondoka awali. Msimu huu Tuanzebe amerejea Villa kwa mkataba wa mkopo.

Toka amerudi Villa Park, Axel hana uhakika wa namba. Anasugua benchi toka wakati wa Dean Smith na sasa Steven Gerard. Muda umewadia, Axel ananukiwa kule Maradona Stadium.

Imeripotiwa kuwa, Napoli wamefikia makubaliano ya mdomo kati yao na Manchester United kuhusu kumsajili Tuanzebe kwa makataba wa mkopo (mpaka mwisho wa msimu). Dau la €500k limekubaliwa kati ya vilabu hivi na huenda, Axel akaenda Italia muda wowote ndani ya mwezi huu.


KUWA MILIONEA MSIMU WA SIKUKUU NA SAHARA RICHIES

Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.